• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:55 PM
Ogiek, Ndorobo waomba kikao na Rais kuhusu ardhi

Ogiek, Ndorobo waomba kikao na Rais kuhusu ardhi

Na Tom Matoke

FAMILIA 3,000 za jamii za Ogiek na Ndorobo sasa wanataka kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kumuomba awasaidie wapate makao na kulipwa fidia Jamii hiyo ilitumuliwa kutoka misitu ya umma kaunti ya Nandi wakati wa serikali ya Rais Mwai Kibaki mwaka wa 2006.

Familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwenye baridi kwa miaka 15 iliyopita zinasema kwamba zimekuwa zikipitia hali ngumu tangu walipofurushwa na Shirika la Huduma ya Misitu ya Kenya (KFS) na nyumba zao zikachomwa.

Walilamika kuwa Rais Kenyatta na Naibu Wake William Ruto walipokuwa wakifanya kampeni mwaka wa 2013, waliahidi kushughulikia masaibu yao lakini hawajafanya hivyo tangu walipoingia mamlakani.

“Wakati Ogiek na Ndorobo walipofurushwa kutoka msitu wa Cherengonik mwaka wa 2006, serikali iliahidi itahakikisha wanapata makao baada ya kuwatambua waathiriwa halisi. Sasa ni miaka 15 na hakuna lililofanyika,” alieleza msemaji wa jamii hizo Paul Koech.

Bw Koech alisema tayari wametengwa miongoni mwa jamii za Wakalenjin na kufurushwa ni moja ya masaibu mengi yanayowakabili.

Walisema kwamba wale hawana ardhi wanalazimika kuzika wapendwa wao kando ya barabara.

Wanalaumu serikali kwa kukataa kuwapa makao licha ya kuagizwa kufanya hivyo na Mahakama.

You can share this post!

‘Jicho Pevu’ ashambulia familia ya Gavana Joho

Wafungwa waachiliwa kupunguza msongamano