• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 4:55 PM
Pasipoti: Kindiki aendelea kuvunja makateli wa Nyayo House

Pasipoti: Kindiki aendelea kuvunja makateli wa Nyayo House

NA WANDERI KAMAU

WAZIRI wa Usalama wa Ndani, Prof Kindiki Kithure alikita kambi katika Jumba la Nyayo jijini Nairobi mnamo Ijumaa, hii ikiwa siku ya pili mfululizo, kufuatilia taratibu za utoaji pasipoti na stakabadhi nyingine muhimu kwa Wakenya.

Hatua yake inafuatia vilio vya Wakenya kuhusu ucheleweshaji wa utoaji wa stakabadhi hizo na mtindo wa uitishaji hongo, ambao umekolea miongoni mwa maafisa wa Idara ya Uhamiaji katika Jumba hilo.

Baadhi ya Wakenya wamekuwa wakilalamika kuwa pasipoti zao zimekuwa zikicheleweshwa kutolewa kwa hadi miezi sita, licha ya taratibu zilizowekwa kuihitahi idara hiyo kutoa stakabadhi hizo kwa hadi muda wa siku 21.

Prof Kindiki aliapa kuendelea kukita kambi katika jumba hilo hadi pale hali ya kawaida itarejea.

“Kwa siku ya pili, nilifuatilia shughuli katika Idara ya Uhamiaji ambapo tumepata mafanikio makubwa. Kama nilivyotoa agizo mnamo Alhamisi, hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kusimama ovyo katika au karibu na jumba hilo. Maafisa wa usalama watahakikisha sheria na kanuni zilizowekwa zimefuatwa. Watamkamata mtu yeyote atakayepatikana akiitisha hongo,” akasema Prof Kindiki.

Waziri aliwashauri Wakenya wanaotuma maombi ya kupata stakabadhi hizo kutotoa hongo yoyote.

“Ili kuharakisha taratibu za utoaji pasipoti na stakabadhi nyingine, tumebuni vitengo maalum kuhakikisha stakabadhi zinazohitajika kwa dharura zimetolewa kwa haraka,” akasema.

Prof Kindiki alisema kuwa pasipoti 44,000 zilizo katika Idara hiyo zitatolewa kwa muda wa siku 14 zijazo.

Alisema kuwa serikali itaitengea idara hiyo Sh1.3 bilioni katika mwaka wa kifedha wa 2023/24 ili kuiwezesha kununua mitambo mipya ya kuchapisha na kutoa stakabadhi hizo.

  • Tags

You can share this post!

Tumeweka WiFi mpate kazi za kidijitali, serikali yaambia...

Betty Njeri: Mkome kutembea na pini za kutia pancha penzi...

T L