• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Sh100m kutumika kujenga shule zilizoharibiwa na majangili

Sh100m kutumika kujenga shule zilizoharibiwa na majangili

NA SAMMY LUTTA

SERIKALI ya kitaifa imetenga Sh100 milioni katika bajeti yake ya ziada kwa lengo la kujenga shule ambazo zimebomolewa au kuteketezwa na majangili katika eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Mnamo Jumanne, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alihimiza wabunge kutoka maeneobunge yaliyoathirika kutambulisha wanakandarasi waliofuzu katika kaunti za Turkana, Baringo, West Pokot, na Elgeyo Marakwet, zilizotajwa kama maeneo hatari, ili miradi hiyo itekelezwe.

“Tunataka shule zote zilizoharibiwa na majangili zikarabatiwe upesi ili watoto wetu waweze kuendelea na masomo yao,” alisema Bw Machogu.

Alikuwa ameandamana na aziri wa Maeneo Kame na Maendeleo Kimaeneo, Rebecca Miano.

Miongoni mwa shule zilizoathiriwa ni Kaakong, Nakuse, na Lokwar.

  • Tags

You can share this post!

Hatima ya Matiang’i iko mikononi mwa DPP Haji

Wabunge kuanzisha uchunguzi kuhusu miili iliyotupwa Mto Yala

T L