• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Simu ya kifo

Simu ya kifo

Na RICHARD MUNGUTI

SIMU ya saa tano usiku wa Aprili 17, 2020, kutoka kwa mwanamke ilisababisha mauti ya mume wa Zaitun Abdul, mahakama imeambiwa Jumatatu.

Baada ya kuzugumza mambo ya mahaba na mpiga simu, mumewe Zaitun alianza vurugu na hiyo ndiyo ikawa siku yao ya kurushiana cheche za maneno.

Mahakana ya Milimani imefahamishwa Jumatatu kwamba usiku huo wa Aprili 17 ulikuwa wa raha lakini ukageuka kuwa wa majonzi Zaitun alipoangamiza maisha ya mumewe.

“Wawili hao walikuwa wanazozana huku kila mmoja akidai mwenzake sio nwaminifu,” Mahakama imefahamishwa.

 

Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Milimani Carolyne Muthoni Nzibe. Picha/ Richard Munguti

Kisa hicho kilichotokea katika mtaa wa mabanda wa Lindi, Kibra katika Kaunti ya Nairobi kiliwaacha wengi na mshangao.

Hakimu mkazi Carolyne Muthoni Nzibe amefahamishwa na viongozi wa mashtaka Winnie Moraa na Angela Fuchaka kwamba mkurugenzi wa mashtaka ya umma hajaamua shtaka atakalomfungulia Zaitun.

Mahakama imeamuru Zaitun arudishwe rumande hadi Mei 7 kuwezesha DPP kuamua shtaka atakalofunguliwa.

“Utarudishwa rumande hadi Mei 7, 2020, DPP aamue shtaka utakalofunguliwa,” Bi Nzibe amemweleza mshtakiwa.

You can share this post!

Ashtakiwa kumuua mpenziwe kwa kutofautiana nani alifaa...

Guardiola hataki Messi atoke Barcelona

adminleo