• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 2:18 PM
TUM kuanza kutoa mafunzo ya udaktari

TUM kuanza kutoa mafunzo ya udaktari

Na KENYA NEWS AGENCY

ENEO la Pwani hatimaye limepata chuo cha kwanza cha kutoa mafunzo ya taaluma ya udaktari baada ya kukamilika kwa ujenzi wa shule ya utabibu katika Chuo Kikuu cha Technical (TUM) jijini Mombasa.

Shule hiyo yenye jengo la orofa nne, ambayo ujenzi wake ulianza Aprili 7, 2017, imeanza kutoa kozi za shahada katika udaktari na upasuaji miongoni mwa kozi nyingine.

Shule hiyo mpya inajumuisha maabara sita, vyumba 18 vya madarasa, chumba cha kuhifadhi maiti, maktaba, maabara ya kompyuta, ofisi saba, mkahawa na maegesho.

Naibu Chansela wa TUM, Profesa Leila Abubakar alisema wapo tayari kuwasajili kikundi cha kwanza cha madaktari 560 na kuwapa mafunzo ifikapo Septemba mwaka huu baada ya kuweka vifaa na samani za jengo hilo.

“Shule yetu mpya ya dawa itawasajili wanafunzi 560 Septemba 2022. Tulipokea Sh12 milioni kutoka kwa mshirika wa Ubelgiji na tunatafuta usaidizi zaidi kutoka kwa washikadau,” akasema profesa Abubakar.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wakamata 4 wanaoshukiwa kula na kuuza nyama ya...

Jinsi ya kusafisha meko na ovena

T L