• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
UCHAMBUZI WA FASIHI: Jinsi ya kujibu Maswali kuhusu wahusika na ploti

UCHAMBUZI WA FASIHI: Jinsi ya kujibu Maswali kuhusu wahusika na ploti

WAHUSIKA ni watu au vitu ambavyo hujenga maudhui ya yale yanayorejelewa katika riwaya ya Chozi la Heri.

Sifa za wahusika zinastahili kuandikwa kwa uyakinifu; mwanafunzi asitumie vikanushi kwa mfano, asitumie maneno kama hana utu (ni katili), si mwaminifu (ni mkware). Mtahini akitumia vikanushi kwa sifa za mhusika,basi atafeli.

SIFA ZA WAHUSIKA

Sifa za mhusika zitajulikana kwa kurejelea:

Yale anayotenda kwa mfamo Ridhaa ni mlezi mwema kwa kurejelea jinsi alivyomshughulikia Mwangeka aliporudi.

Anayosema: Ridhaa tunajua ni msomi kutokana na yeye kutujuza baada ya kuitwa mfuata mvua, alijisimika katika kusoma hadi akawa tabibu.

Anayofikiria kwa mfano: ni mwenye utu- anafikiri jinsi alivyoenda kumsaidia mhasiriwa wa vita baada ya uchaguzi ,anapoiacha familia yake na baadaye kufishwa.

Yale wahusika wengine wanasema kumhusu kwa mfano ni mhafidhina pale ambapo Mwangeka anapoadhibiwa kwa kuigiza miviga ya mazishi ya Dede na yale mwandishi anasema kumhusu mhusika anayerejelewa kwa mfano sura ya tatu katika riwaya, mwandishi anatujuza sifa za vijana wenye utu baada ya kuwashughulikia wahasiriwa wa vita vya baada ya uchaguzi.

Jina la mhusika linafaa liandikwe kama lilivyo katika kitabu (Chozi la Heri).

Sifa za Ridhaa ni;

Mwenye bidii; ni daktari ambaye alifanya kazi kwa uadilifu.

Mwenye uhusiano mwema; anakula pamoja na majirani.

Mshirikina; anahusisha milio ya bundi na jambo baya kutokea.

Karimu; anasaidia jamii kwa kujenga hospitali.

Mvumilivu; anavumilia kuona mabaki ya kuteketezwa kwa familia yake.

UMUHIMU WA WAHUSIKA

Umuhimu wa wahusika huhusisha mhusika anaeleleza maudhui yapi. Kwa mfano, Mzee Kedi ni kielelezo cha watu katili katika jamii – anasababisha mauaji ya familia ya Ridhaa. Ni kielelezo cha watu baguzi – inasemekana kuwa licha ya Ridhaa kuishi nao kwa miongo mitano, bado alionekana mgeni huko Kalahari.

Pia wahusika hujenga wahusika wengine. Kutokana na maelezo ya wahusika fulani, tunajuzwa sifa zao. Kwa mfano, kupitia kwa Ridhaa, tunatambulishwa kwa mhusika Tila ambaye ni:

Mtambuzi – anatambua kuwa licha ya kuwa yeye si mpiga kura, Mwekevu angemshinda mpinzani wake kwa asilimia kubwa.

Mzalendo – Tila alitazamia kusoma na kuwa wakili ili awashughulikie wananchi ambao walihasirika kwa sababu ya uongozi mbaya wa viongozi walikuwepo mamlakani.

PLOTI

Wahusika hujenga ploti ya riwaya. Mawanda ya riwaya yanatukia kwa kurejelea mtiririko mwafaka wa vitushi, matumizi ya mitindo maalum kama vile nyimbo, masimulizi na matumizi ya barua.

ZOEZI LA TATHMINI

Eleza umuhimu wa Selume katika kujenga ploti na maudhui ya Riwaya hii.

Joyce Nekesa

Kabsabet Boys High School

You can share this post!

Bodaboda 16 washtakiwa kwa kudhulumu mwanamke jijini

Man-City waingia robo-fainali za UEFA licha ya Sporting...

T L