• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Wakorino waomba wasivae helmeti wakisema ni dharau kwa imani yao

Wakorino waomba wasivae helmeti wakisema ni dharau kwa imani yao

Na KNA 

Chama cha waumini wa dhehebu la Akorino eneo la Mbeere Kusini, kimemuomba waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i kuwaruhusu wanachama wa madhehebu hiyo wasivalie kofia za usalama.

Mwenyekiti wa Mbeere South Akorino Association Askofu Patrick Munyi, alisema ni kinyume cha imani yao kuvalia helmeti au kofia ya aina yoyote juu ya vilemba vyao.

“Ni kinyume cha imani yetu kuvalia chochote juu ya vilemba vyetu na tunamuomba waziri kusikiliza kilio chetu,” alisema Bw Munyi.

Aliongeza kuwa chama hicho kinataka sheria za Michuki zitekelezwe kikamilifu ili kupunguza ajali za barabarani ambazo zimeongezeka nchini.

Askofu Munyi alipongeza muafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, akisema umeleta amani nchini ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi.

“Tunaamini muafaka huo ni jibu la maombi tuliyotoa kwa Mungu Machi 19 mwaka huu amani iweze kudumu nchi ilipokumbwa na msukosuko wa kisiasa,” alisema.

Alisema hayo alipoongoza ibada ya kutoa shukrani kwa amani inayoshuhudiwa nchini.

 

You can share this post!

Breki kwa ada mpya ya nyumba kukatwa kwa mishahara

Tutasambaratisha masomo Januari ‘uhamisho...

adminleo