Lofa aonywa kutumia choo cha jirani, apewa siku tatu kukijenga chake
LOFA mkazi wa hapa alipewa siku tatu kujenga choo chake la sivyo achukuliwe hatua.
Duru zinasema jirani wa kalameni alikuwa akilalamika kuhusu vitendo vya polo kutumia choo chake.
“Huyu jamaa kila siku asubuhi akiamka lazima nikutane naye akija kutumia choo changu ama akiondoka,” jirani alilalamika.
Jirani alimuonya polo dhidi ya kuendelea kutumia mali yake.
“Juzi ulinifanya nikasubiri nje kwa muda mrefu wewe ukiwa unajisaidia ndani ya choo changu. Acha kuleta msongamano kwangu. Jenga choo chako la sivyo nikuchukulie hatua,” jirani alimzomea polo.
Majirani wengine waliungana na kumuonya polo kukoma tabia hiyo.