Wawili wafa, watatu wakijeruhiwa kwenye ajali Kirinyaga
WATU wawili walifariki na wengine watatu kujeruhiwa kwenye visa tofauti vya ajali Kaunti ya Kirinyaga.
Ajali ya kwanza ilifanyika mwanamke alipogongwa akivuka barabarani kijiji cha Riandira, eneobunge la Ndia.
Alikuwa akielekea sokoni alipogongwa na gari hilo na mwili wake umehifadhiwa kwenye makafani ya Kerugoya.
Ajali ya pili ilitokea pikipiki mbili zilipogongana kwenye kijiji cha Kibirigwi. Kwenye ajali hiyo mmoja wa waliokuwa wakiendesha pikipiki aliaga dunia papo hapo na mwili wake ukapelekwa mochari ya Karatina.
Kwenye kijiji cha Murubara, watu watatu walijeruhiwa matatu ilipogongana na lori. Lori lilikuwa likielekea Makutano kutoka Embu dereva alipopoteza mwelekeo na kugonga matatu ambayo ilikuwa ikitokea upande wa pili.
Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini kwa matibabu. Lori na gari hilo lilibururwa hadi kituo cha polisi cha Wangúru kukaguliwa