Habari Mseto

Vivukio 11 kujengwa kwenye barabara ya Outering

April 18th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Ujenzi wa vivukio vya wakazi wa Nairobi wenye kutembea kwa miguu katika Barabara ya Outering umeanza.

Hii ni baada ya wakazi wa Nairobi kuzusha hasa kwa sababu ya ongezeko la ajali katika barabara hiyo.

Jumla ya vivukio 11 vinatarajiwa kujengwa na kampuni ya Uchina, Sinohydro Tianjin Engineering kwa gharama ya Sh880 milioni.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Barabara za Jiji (KURA). Katika taarifa, KURA ilisema ujenzi wa vivukio hivyo ulikuwa ukiendelea.

 “Tunaomba wananchi kuwa wavumilivu tunapoendelea kutia juhudi kuimarisha usalama barabarani,” ilisema KURA katika taarifa hiyo.

Kivukio kimoja kitajengwa kwa gharama ya Sh80 milioni katika barabara hiyo ya kilomita 13 inayoanzia mlimokuwa Taj Mall hadi Allsops, katika Barabara Kuu ya kuelekea Thika.