Mamaye Hamisa alia bintiye kuitwa ‘wa kando’ na Diamond

Na PETER MBURU

MSANII Diamond Platnumz kutoka Bongo aliibua cheche za maneno pale alipomrejelea kichuna Hamisa Mobetto kuwa ‘wa kando’, na mwanaye Dylan kuwa ‘mwanaharamu’ kwenye video iliyosambaa mitandaoni.

Katika video hiyo inayodaiwa kuwa ya mahojiano kati ya Diamond akiwa Nigeria, msanii huyo anasikika akijilaumu kuwa 2017 ulikuwa mwaka mbaya kwake.

Alisema ni mwaka huo ambapo alichezea penzi lake na mpenzi wake wa muda mrefu Zari Hassan, na Hamisa Mobetto.

Mwishoni mwa kanda hiyo, Diamond anawashauri watu walio na mipango ya kando kuwa makini na wawe wakitumia kondomu ili kuzuia kuwapa mimba mipango ya kando kama alivyofanya yeye.

Lakini semi hizi za msanii huyo hazikupokelewa vyema na mamake Hamisa Mobetto, Bi Shufaa Lutiginga, ambaye sasa amesema zilimchoma rohoni.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Bi Shufaa alisema hangependa hata kuyasikia mambo hayo tena kutokana na uchungu yaliyompa.

“Jamani inauma na kwa kweli nisingependa hayo mambo jamani kuyaongelea mimi… jamani naombeni sana mtafuteni huyo mwenyewe aliyesema au Mobeto tafadhali, niacheni mimi nipumzike,” akasema Bi Shufaa.

Habari zinazohusiana na hii

Comments

  • ian boy

    02/20/2020

    si vzuri hata kidogo kumdharau mtu uliyefanya nae mapenz kbla ya kuwa na mwengine kama diamond platnumz alivomfanyia zari namshawishi zari asikubal mwili wake uchezewechezewe hivi hivi kwani wakenya watuonya kwa kusema “don’t allow any boy to make practiz with your vigina” Najua inauma kwly kuachwa n mpnz wako wa dhat mliyependana xana ipo cku diamond utatendwa ahakujifanya coz we n billioner nltendwa pia mm n dem mmoja nliekutana naye kwa disco moja apa mtaan vragon dem alinibwagia cheche za matusi huku akxema kuwa nlkuwa na madem wengi mtaan

  • Anonymous

    12/20/2018

    Wachana nayeye hakuche kenya wawaje kumsuhiya sio poa

Leave a Reply