• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 6:50 AM
Swazuri alilia mahakama impunguzie joto

Swazuri alilia mahakama impunguzie joto

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Ardhi Prof Mohammad Swazuri Jumatano alieleza korti kwamba hajakabidhiwa nakala za ushahidi katika kesi inayomkabili ya kulipa kwa njia ya ufisadi wamiliki wa ardhi iliyonunuliwa na shirika la reli nchini kujenga reli mpya Sh221 milioni.

Prof Swazuri aliomba mahakama iahirishe kesi hiyo dhidi yake kwa vile hajakabidhiwa nakala za mashahidi.

“Naomba hii kesi iahirishwe kwa vile washtakiwa hawajapewa nakala za mashahidi na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma,” Prof Tom Ojienda anayemwakilisha mwenyekiti huyo alisema.

Aliomba korti iwatengee siku ya karibu ya kusikizwa kwa kesi hiyo ndipo “waone ikiwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP Noordin Haji anawachezea watu ama yuko na ushahidi dhidi ya washukiwa.”

Anataka Afisi ya DPP na mawakili wanaowatetea washtakiwa wafanye kikao Septemba 6 waafikiane kuhusu ushahidi huo.

Na wakati huo huo Prof Swazuri alikubaliwa kurudi afisini chini ya ulinzi mkali.

Alliruhusiwa na hakimu mkuu Bw Lawrence Mugambi.

You can share this post!

Ajabu ya mteja kuwa na mawakili 32

Kesi ya Mwilu yavutia wanahabari kutoka kona zote za dunia

adminleo