• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 3:55 PM
Nitazidi kuhudumia wakazi wa Nairobi kutoka Machakos – Sonko

Nitazidi kuhudumia wakazi wa Nairobi kutoka Machakos – Sonko

Na STEPHEN MUTHINI

GAVANA wa Kaunti ya Nairobi Mike Sonko amekejeli makataa ya madiwani wa bunge la kaunti kumtaka akome kuhudumia wakazi wa jiji kutoka nyumbani kwake Mua Hills, Kaunti ya Machakos na kurejea kwa ofisi yake Nairobi.

Bw Sonko alisema hawezi kutishwa na yeyote na atazidi kutekeleza majukumu ya ugavana akiwa mashinani.

“Ukiendesha gari kutoka Nairobi hadi Mua Hills itakuchukua dakika 25 pekee. Siondoki hapa kwa kuwa hapa ni nyumbani kwangu.

Hata Rais mwenyewe huhudumia wananchi kutoka nyumbani kwake Ikulu ya Nairobi, si wakati wote anafika ofisini kwake katika Jumba la Harambee,” akasema gavana huyo alipohutubia wanahabari nyumbani kwake. Bw Sonko alisema haijalishi pahali anapofanyia kazi, cha muhimu ni kuwahudumia wakazi wa Nairobi kwa njia inayowaridhisha.

Madiwani wa kaunti yake hapo Alhamisi walimpa siku 14 kurejea ofisini katika jumba la City Hall, wakionya kumuita kuelezea bunge la kaunti sababu za kutoroka ofisini.

Lakini Bw Sonko amekuwa akiendesha shughuli za jiji la Nairobi kutoka nyumbani kwake tangu Mei mwaka huu, wakati alidai alikuwa amepokonywa walinzi.
Alisema amekuwa akishirikiana na madiwa na amekuwa akizuru wadi kadhaa za jiji kuzindua miradi ya maendeleo.

Aliwataka wawakilishi wa kaunti wadhubutu kupiga kura ya kukosa Imani naye, akisema kuna njia mbadala za kubatilisha uamuzi wao.

Gavana huyo pia alipuuzilia mblai wita wa bunge la kaunti kumtaka ateue Naibu Gavana, akisema yeye tayari ashafuata ushauri wa Mahakama ya Juu.

“Ushauri wa mahakama ya juu ulikuwa wazi kwamba niteu naibu wangu katika kipindi cha siku 14. Nilifanya hivyo na nikamteua wakili Dkt Miguna Miguna ambaye bunge la kaunti lilimpuuza,” akasema Bw Sonko akiongeza kuwa hajui suluhu baada ya madiwani kukataa chaguo lake.

Aliambia wanahabari kuwa huenda akarejea kwa Mahakama ya Juu kupata ushauri zaidi kuhusu suala la uteuzi wa naibu gavana.

Alijitetea kuwa hafai kulaumiwa kwa kuwa baada ya Dkt Muguna kukataliwa, aliwateua watu wengine wane kujaza nafasi hiyo.

You can share this post!

Niite nikufundishe jinsi ya kukabili madeni, Raila amwambia...

Joho akumbana na ghadhabu za wakazi kwa kuongeza ushuru

adminleo