• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Joho akumbana na ghadhabu za wakazi kwa kuongeza ushuru

Joho akumbana na ghadhabu za wakazi kwa kuongeza ushuru

Na WINNIE ATIENO

Serikali ya Kaunti ya Mombasa Jumamosi ilijipata taabani kufuatia kodi ya gharama ya juu kwenye Mswada wa Fedha wa 2018/2019 huku wafanyabiashara wakisema itawaadhibu.

Hata hivyo, wasimamizi wa kaunti walijitetea wakisema ili wakazi na wafanyabiashara wapate maendeleo na huduma bora ni sharti walipe ushuru.

Wakazi hao waliokuwa na hasira walimiminika kwenye ukumbi wa Tononoka na kutoa maoni yao huku wengi katika sekta ya utalii, mazingira na watu wanaoishi na ulemavu wakiipinga na kutaka mabadiliko.

Kwa mfano, walemavu walisema walifurushwa kwenye jiji la Mombasa ambako walikuwa wanajitafutia riziki, hata hivyo afisa wa fedha Abdulwahab Mbarak akisema hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia msongamano kati kati ya jiji hilo la kitalii.

“Lakini Mswada wa Fedha ni afueni kwenu manake tumewapatia kipaumbele, tutawatafutia sehemu ya kufanya biashara,” akaahidi Bw Mbarak.

Wakitoa maoni yao, wakazi waliitaka bunge la kaunti akiongozwa na spika Harub Khatri kupinga mswada huo wa kifedha.

“Fanyeni marekebisho kabla mupitishe mswada huu wa fedha ambao utatuadhibu kama wafanyabiashara,” akasema Teresia Ndirangu.

Wakazi, wafanyabiashara, makundi ya wanawake na vijana, watetezi wa haki za binadamu walitoa wito kwa wawakilishi wa wadi akiongozwa na spika wa bunge la kaunti hiyo Bw Harub Khatri kuipinga.

Lakini wasimamizi wa kaunti walitetea mswada huo wakisema utaboresha huduma za Mombasa.

“Tuna hadi Septemba 26, kabla mswada huu upitishwe bungeni hadi wakati huo mnafaa kutoa maoni msijali hata hivyo wawakilishi wa wadi watapokea maoni yenu,” akasema afisa wa fedha Asha Abdi.

You can share this post!

Nitazidi kuhudumia wakazi wa Nairobi kutoka Machakos...

UKATAJI MITI: Bei ghali ya mafuta inavyotishia misitu

adminleo