• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 5:54 PM
Kibaki amsifu marehemu Godia kama mwanamageuzi

Kibaki amsifu marehemu Godia kama mwanamageuzi

Na BENSON MATHEKA

Rais Mstaafu Mwai Kibaki amemtaja aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Elimu marehemu Prof George Godia kama mtaalamu na mwanamageuzi.

Prof Godia alikufa Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwenye rambirambi zake, Bw Kibaki alisema marehemu Godia atakumbukwa kama mtaalamu shupavu aliyehudumu katika sekta tofauti kwa kujitolea.

“Utaalamu wake umeacha kumbukumbu isiyoweza kufutika. Ninaomba Mungu aipe familia yake amani na faraja,” alisema Mzee Kibaki kwenye taarifa.

Kibaki alimteua Godia kuwa katibu wa wizara ya elimu katika serikali yake 2014.

Naibu Rais William Ruto alisema marehemu Godia atakumbukwa kama msomi na mwanadiplomasia mtajika.

“Ninafariji familia, marafiki na wasomi kufuatia kifo cha Prof George Godia. Godia alitetea maslahi ya Kenya kote ulimwenguni,” alisema Bw Ruto.

Godia alijiunga na wizara ya elimu 2004 kuwa katibu wa elimu na kupanda cheo kuwa katibu wa wizara.

Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi pia alituma rambirambi zake kwa familia ya Prof Godia akisema alifanya kazi yake kwa kujitolea na utaalamu mkubwa.

You can share this post!

Ufisadi ndio kiini cha njaa Afrika – Wataalamu

KURUNZI YA PWANI: Wanawake wa jamii ya ufugaji wakumbatia...

adminleo