• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Serikali kuongeza ada ya NHIF

Serikali kuongeza ada ya NHIF

Na BERNARDINE MUTANU 

Serikali imependekeza wafanyikazi walio na mishahara ya juu kuanza kukatwa zaidi kwa mchango wao katika Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Matibabu (NHIF).

Kulingana na Waziri wa Afya Bi Sicily Kariuki, serikali itakubaliana na wafanyikazi na waajiri kutekeleza hatua hiyo, ambayo awali ilipingwa na Muungano wa Vyama vya Wafanyikazi (COTU).

Pendekezo hilo limetolewa chini ya miaka mitatu baada ya NHIF kuongezea wafanyikazi kiwango cha mchango wao kutoka Sh320 hadi kati ya Sh500 na Sh1,700 kuambatana na kiwango cha mshahara.

“Kutokana na kuwa lilipingwa kwanza, lazima tushirikishe wafanyikazi, waajiri na umma katika mazungumzo,” alisema Bi Kariuki.

Katika mazungumzo hayo, waajiri wanawakilishwa na FKE nao wafanyikazi wanawakilishwa na COTU, mashirika ambayo yana nyadhifa katika bodi simamizi ya NHIF.

 

 

 

You can share this post!

Safari za moja kwa moja kutoka Doha hadi Mombasa zaanza

Bei ya stima haitapanda kwa sababu ya ushuru mpya

adminleo