• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:21 PM
Mtakiona mkipandisha bei ya unga, serikali yaonya wafanyabiashara

Mtakiona mkipandisha bei ya unga, serikali yaonya wafanyabiashara

Na BERNARDINE MUTANU 

Wauzaji wa unga wameonywa dhidi ya kupandisha bei ya bidhaa hiyo kwa kusingizia ushuru wa asilimia 16 unaotozwa mafuta. 

Akiongea na wanahabari Jumanne, Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri alidai kuwa ushuru huo hauna athari kwa watengenezaji wa ungahivyohawafai kuongeza bei ya unga. 

Hata hivyochama cha wasagaji wa unga(CMA) tayari kimeonya kuwa kitaongeza bei ya unga kwa sababu ya ongezeko la bei ya mafuta. 

Bei ya juu ya mafuta inaathiri gharama ya usafirishaji sio tu wa mahindilakini pia unga uliosagwa. 

Waziri huyo alisema kiwango cha mahindi yaliyovunwa nchini kimo juu ikilinganishwa na msimu uliopitahivyo hakuna upungufu wa mahindi. 

Alisema msimu huu magunia milioni 46 yatavunwa ikilinganishwa na magunia milioni 40 yaliyovunwa msimu 

You can share this post!

Mkurugenzi aliyejiuzulu kusalia ofisini kwa miezi 6

Zimbabwe si kama Kenya, Mnangagwa amuonya Chamisa

adminleo