• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Taharuki Malindi maskwota wakijigawia shamba

Taharuki Malindi maskwota wakijigawia shamba

Na CHARLES LWANGA

TAHARUKI imetanda katika shamba la ekari 900 la ukulima la ADC huko Kisiwani eneo la Sabaki, Kaunti ya Kilifi baada ya kundi la maskwota takriban 300 kuvamia na kugawanya shamba hilo.

Maskwota hao pia walifunga barabara kuu ya Malindi-Lamu na kuwasha moto huku wakitatiza uchukuzi.

Wakiongozwa na diwani wa eneo hilo, Bw Edward Kazungu Delle walisema wameamua kuchukuwa shamba lao kutoka kwa mabwenyenye ambao wanadaiwa kuungana na usimamizi wa shamba hilo la ADC kulinyakua.

“Leo tumeingia na kuchukua shamba letu baada ya kufika kikomo, hii ni kwa sababu Tume ya Kupambana na Ufisadi (EACC), Tume ya Ardhi (NLC) na Kiongozi wa Mashtaka (DPP) wamekosa kusikiza malamishi yetu,” alisema.

Kampuni ya Maji na Maji taka Malindi (Mawasco) tayari imenunua ekari 25 katika shambani hilo kwa Sh40 milioni ili kujenga nyumba za wafanyakazi wake.

Mkurugenzi Mkuu wa Mawasco, Bw Gerald Mwambire jana alikanusha madai kuwa kampuni yake ni baadhi ya kundi lenye njama inayotumiwa kunyakuwa shamba hilo la ADC akisema wanamiliki shamba hilo kihalali.

Alisema baadhi ya maskwota wanaoishi mahali hapo walifidiwa Sh2.5 milioni na hawana ubaya na mradi huo ambao pia unanuia kujenga barabara, kituo cha mafuta na shule.

Lakini jana maskwota waliojihami kwa jembe, panga na matawi, walivamia shamba hilo na kujigawia kabla ya kufanya utamaduni wa wafu wa jamii ya Mijikenda ili kukumbuka mababu wao waliozikwa shambani humo.

Bw Stembo Kaviha, mkurugenzi mkuu wa wakazi wa Sabaki alisema maskwota karibu 27,000 eneo hilo wana ushahidi wa kutosha kuwa shamba hilo limeibwa na mabwenyenye kutoka Rift Valley.

“Leo tuna hasira kama nyoka kwa sababu serikali imekosa kusikia kilio chetu cha kusimamisha wizi wa shamba hili,” alisema na kuongeza kuwa “hakuna yeyote aliyefidiwa kama vile wengine wanavyodai.”

imekosa kusikia kilio chao kwa sababu wao ni watu maskini kutoka pwani wanaodaiwa kuwa wanyonge miongoni mwa wengi.

“Rais Uhuru Kenyatta yuko mbeleni kupambana na ufisadi na jambo hili la unyakuzi wa shamba la ADC halifai kupuuzwa,” alisema na kuongeza “usimamizi wa shamba la ADC unafaa uchunguzwe kutokana na ufisadi.”

Pia, Bw Delle aliuliza ni kwa nini tume ya NLC inawazuia maskota kuvamia shamba hilo wakati mabwenyenye wanavamia na kujenga ukuta shambani humo.

“Tume ya NLC inatuzuia kwa sababu sisi ni maskini, sisi na umaskini wetu sasa tumeamua kuchukuwa shamba letu,” alisema.

Wiki iliyopita, Tume ya NLC ikiongozwa na mwenyekiti msimamizi Abigael Mbagaya alipokuwa anachunguza umiliki wa ardhi eneo Kaunti ya Kilifi huko Watamu, alikashifu maskota kutokana na uvamizi wa shamba za umma.

You can share this post!

Ujenzi wa kiwanda cha pombe cha Sh15B Kisumu wakamilika

DPP ataka mnajisi aozee jela maisha sio miaka 20

adminleo