• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Unaweza kumtambua msagaji kwa kutazama vidole vyake – Utafiti

Unaweza kumtambua msagaji kwa kutazama vidole vyake – Utafiti

BBC na PETER MBURU

UREFU wa vidole fulani vya mikono unaweza kuamua hali ya mapenzi kwa wanawake, wawe wakishiriki mapenzi  kikawaida ama kuwa wasagaji.

Hii ni kulingana na utafiti wa kisayansi, ambao umeonyesha kuwa tofauti ama usawa wa urefu wa vidole vya kwanza na chanda kwenye mkono wa kushoto wa mwanamke unaweza kuwa na maana kibayolojia na kuashiria hali ya mapenzi.

Walipofanya utafiti, wanasayansi walibaini kuwa kati ya wanawake 18 ambao ni pacha, wale waliokuwa wasagaji walikua na tofauti za urefu kati ya vidole vya kwanza na chanda.

Kwa upande mwingine, wanawake wanaoshiriki mapenzi kikawaida walikua na usawa wa urefu wa vidole hivyo.

Hii, kulingana na watafiti hao ni kutokana na chembechembe za uanaume walizopata wanawake hao walipokuwa tumboni, kwa jina Testosterone.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Essex walisema wasagaji walipokea kiwango kikubwa cha testosterone walipolinganishwa na wanawake walioshiriki mapenzi ya kawaida, wakati walipokuwa tumboni.

Hata hivyo, hali hii ilikuwa tu katika mkono wa kushoto na ni ishara iliyoko kwa wanawake pekee. Walipofanyia wanaume 14 pacha utafiti uo huo, hali yenyewe haikujirudia.

Kulingana na wanasayansi hao, watu hupokea chembechembe hizo za testosterone wawapo tumboni, lakini kiwango chake hutofautiana.

“Utafiti umeonyesha kuwa hali zetu za mapenzi huamuliwa tumboni na hutegemea kiwango cha chembechembe za uanaume tunazopokea na namna mili yetu inazipokea. Wanaopokea nyingi za uanaume wana uwezekano mkubwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja,” akasema mtafiti Dkt Tuesday Watts.

Kulingana na mtafiti huyo, kwa kumtazama mtu mikononi tu inawezekana kujua hali yake ya mapenzi.

You can share this post!

Ushahidi dhidi ya mganga wa Kangundo wakosekana, aachiliwa...

BIASHARA: Si haki serikali kuzuilia bidhaa za...

adminleo