Wawaniaji urais Brazil wamenyana mitandaoni
MASHIRIKA Na CECIL ODONGO
BRASILIA, BRAZIL
WAWANIAJI wa Urais wanatumia mitandao ya kijamii kusaka kura ya zaidi ya wapiga kura 147milioni wanaotarajiwa kushiriki uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwezi huu.
Jair Bolsonaro (pichani) ambaye anapigiwa upato kuibuka mshindi amekuwa amekuwa akitangamana na wapiga kura kupitia mitandao ya Facebook, WhatsApp na Twitter huku mpinzani wake wa karibu Fernando Haddad anayewania kupitia chama cha Workers Party akilazimika kujitetea kila mara kutokana na habari feki zinazochipuka kumhusu katika mitandao hiyo.
Maafisa wa polisi nchini Brazil hata hivyo wameanzisha uchunguzi kuhusu habari feki mtandaoni kuhusu wawaniaji hao wawali baada ya wafuasi wao kakabiliana kwa maneno kila moja akilenga kumpaka tope mpinzani.
Matokeo ya kura za maoni nchini humo yanamweka Bolsonaro, 63 kifua mbele kwa asilimia 59 huku Bw Haddad akimfuata kwa asilimia 41.