• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Wanakijiji 300 wakesha kwa kijibaridi kufuatia mzozo wa ardhi

Wanakijiji 300 wakesha kwa kijibaridi kufuatia mzozo wa ardhi

Na OSCAR KAKAI

TAKRIBAN watu 300 wa familia 11 katika kijiji cha Kapsait,kaunti ndogo ya Pokot Kusini, Kaunti ya Pokot Magharibi wanalala kwa baridi kufuatia mzozo wa ardhi ambao umekuwepo kwa muda mrefu.

Familia hizo zimekuwa zikikesha katika hali hiyo kwa wiki moja sasa baada ya kuwachwa bila makao, nyumba zao zilipochomwa,mali ya mamilioni na mazao mashambani kuharibiwa na maafisa wa usalama. Hatua hiyo ilijiri baada ya korti kutoa agizo kuhusiana na mzozo wa shamba baina ya familia za koo mbili na mnununzi Bw Chemer Lochaling’a umekuwepo kwa zaidi ya miaka arobaine wakizozania ekari kumi 11.94 za shamba.

Hali ya wanafunzi wa darasa la nane na wa kidato cha nne ambao ni wanafunzi wa kutwa wakati huu wa mtihani haijulikani sababu hawana chochote cha kutegemea.

Kwa sasa wakazi wanadai kuwa hawakupewa notisi ya korti na sababu ya kufurushwa.

Hii ni mara ya pili kwa familia hizo kufurushwa baada ya kufurushwa tena mwaka wa 2015.

Wahanga hao wanahitaji msaada wa dharura wa chakula,makazi na madawa baada ya kufurushwa kutoka kwenye makazi yao.

Familia hizo ambazo zimewachwa bila makao sasa zimepiga kambi katika vijiji vya Kapsakar na Murkokoi,Lokesheni ya Lelan wanaomba usaidiazi wa chakula kutoka kwa serikali na msalaba wa mwekundu ili waweze kukabiliana na hali yao baada na tukio hilo.

Familia hizo ambazo zina hati miliki za shamba hilo zinadai kuwa wao ndio wamiliki kamili wa ardhi hiyo.

“Polisi walikuja na kuchoma nyumba zetu bila kutupea notisi.Tunalala chini ya miti na tunaishi kwa hofu kutokana na milio ya risassi ya maafisa wa polisi ,”akasema Selina Tong’elech Bi muathirwa.

Walisema kuwa mzozo kati ya makundi hayo mawili uko kortini na wamehindwa ni kwa nini maafisa wa polisi walikuwa wakatili bila kuja na notisi ya korti.

“Kesi bado iko kortini na tunashindwa ni sababu gani wanakuja kutufurusha,”alisema Bi Tong’elech.

Wakazi hao wenye ghadhabu walilalamikia hatua ambayo ilichukuliwa na maafisa wa polisi ambao waliwalazimisha kuchoma nyumba zao na kuumiza waathiriwa kwa kuwapiga marisasi bila kuwajali badala ya kuwalinda.

“Mbona polisi wanafukuza watu na kuwachomea nyumba bila kufuata sheria. Ng’ombe 28 na kondoo 60 wamepotea na hatukamu.Watoto wetu wanalala kwenye kijibaridi . Wanadai kuwa wanataka kuua mtu.Hata majirani wametukataa .Kwani sisi sio wakenya,”aliuza Bi Chenanga’t Cheporiot.

Wakazi hao wanasema kuwa maafisa wa polisi wanatumika na familia hiyo nyingine kuwafurusha bila sababu muhimu.

“Maafisa wa polisi wamehongwa na wapinzani wetu ,”alisema Bi Cheporiot.

Walisema kuwa wanashindwa mbona suala hilo lilitekelezwa bila kuhusisha wakazi wakiwemo machifu na wazee bila kuhusishwa sababu hawajakataa kuondoka ikiwa kesi hiyo itafikia kikomo.

“Hii ni tabia ya kiimla na unyanyasaji kwa wakazi ambao wanamiliki ardhi kihalali.Tumepoteza mali nyingi na stakabadhi za watoto wetu ambao wako shuleni,”alisema Bw Jacob Limatwole .

Familia hizo ambazo zimeathirika zinataka haki itendeke na wanataka serikali kuchukua hatua kwa haraka na kutatua mzozo huo sababu wanaweza kuchukua sheria mikononi mwao na kulipisha kisasi.

“Tunataka serikali kuingia kai suala hili kwa haraka la sivyo tutalipisha kisasi,”alisema Bw Loripo Limara.

Bw Loripo alisema kuwa mali ya mamilioni iliharibiwa ikiwemo mazao kwenye magala ,vyombo vya nyumba ,nguo ,fedha ,stakabadhi sabbau kila kitu kilichomwa na maafisa hao wa polisi.

Kwa sasa wanatoa wito kwa watetekezi wa haki za kibinadamu ,wahusika na viongozi wa eneo hilo kuingilia kati suala hilo.

Bi Esther Arumonyang alisema polisi walitumia nguvu kupita kiasi kufurusha familia hizo .

“Haikufanywa kwa njia ya utu .Watoto wangu wa darasa la nane hawaendi shuleni kufanya mtihani sababu ya hofu. Wako na haki zao.Rais anafa kuingilia kati Uhuru Kenyatta.Serikali ya kaunti haikuja kutusaidia na wacha wakuje watuondoe,”akasema Bi Kachilana Jon stone.

Hata hivyo ,naibu wa kamishina wa kaunti ndogo ya Pokot Kusini Bw Frederick Kimanga kulikuwa na agizo la korti kufurusha familia hizo .

“Kesi ya wazee iliamua kuwa shamba ni la Bw. Chamer,mahakama ya juu iliamua kuwa shamba ni la Chamer,”alisema.

Alisema kuwa maafisa wa polisi waliwapa notisi ya wiki mbili kuondoka kwenye shamba hilo.

Hata hivyo Bw Kimanga alisema kuwa maafisa wa polisi hawafai kutumia nguvu kuoia kiasi kufurusha wakazi hao.

You can share this post!

Polisi auawa na wanakijiji baada ya kumuua mkewe

Bondia aliyemuua kocha wake asukumwa jela miaka 20

adminleo