• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Tabaka la wastani kuzidi kununua umeme kwa bei ya zamani

Tabaka la wastani kuzidi kununua umeme kwa bei ya zamani

Na BERNARDINE MUTANU

Wakenya wa mapato kiwango cha wastani hawatanufaishwa na gharama mpya ya matumizi ya umeme.

Hii ni baada ya Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC) kuwafungia nje katika mageuzi mapya kuhusiana na gharama ya matumizi ya stima.

Kulingana na mageuzi hayo mapya, wananchi ambao hutumia stima kati ya kilowati 10 na 100 walipunguziwa malipo ya umeme kuwa Sh10 kwa kilowati moja.

Ni hatua ambayo ERC ilisema itawafaa sana wananchi ambao wana mapato ya chini, baada ya kuamriwa na Rais Uhuru Kenyatta kufanya hivyo.

Pia, malipo hayo mapya yatawafaa sana wamiliki wa biashara ndogo ndogo katika sekta ya jua kali.

Wakati wa marekebisho ya gharama ya umeme yaliyofanywa miezi mitatu iliyopita, wananchi walio na mapato wastani waliongezewa gharama hiyo kufikia asilimia 54.

Takriban wananchi 517,000 hutumia zaidi ya kilowati 100 kwa mwezi na kutokana na hilo, hawatafaidika kutokana na marekebisho ya hivi punde, ilisema ERC.

You can share this post!

Kioja cha mwaka mwanamume kwenda haja kubwa kitandani kwa...

Mamia ya mifugo wafa baada ya kunyeshewa

adminleo