EACC yaagizwa kumrudishia Kidero mali yake ndani ya saa 72

Na MAUREEN KAKAH

TUME ya Maadili na Kukabiliana na ufisadi (EACC), Jumanne ilipata pigo baada ya Mahakama Kuu kuiagiza iachilie mali yote ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Evans Kidero ndani ya muda wa saa 72.

Jaji Hedwig Ong’udi alitoa agizo hilo katika kesi ambayo Bw Kidero analaumu tume kwa kumnyanyasa kwa lengo la kumlemaza kifedha.

Wakati huo huo, Jaji Ong’udi alimuondoa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kutoka kesi hiyo akisema afisi yake haikuhusishwa na ukiukaji wowote.

“Mali yoyote inafaa kurudishwa katika muda wa saa 72 na msako wowote kusitishwa,” jaji aliagiza.

EACC ilikuwa imevamia mali na mashirika ambayo yanamilikiwa na Dkt Kidero binafsi au washirika wake na kuhangaisha wapangaji na wateja. Aliwasilisha kesi hiyo mwezi jana akitaka maagizo ya kuzuia tume hiyo kutwaa stakabadhi na mali yake ikitumia kibali kilichotolewa Septemba 19.

mali yake. Kesi itatajwa Desemba 6.