• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Wakurugenzi washtakiwa kukwepa kulipa ushuru wa Sh3 bilioni

Wakurugenzi washtakiwa kukwepa kulipa ushuru wa Sh3 bilioni

Na RICHARD MUNGUTI

WAKURUGENZI wawili wa kampuni moja wameshtakiwa kwa kukataa kulipa ushuru wa zaidi ya Sh3.2bilioni miaka miwili iliyopita.

Mabw Dhaval Vinodbhai Soni, Bw Bhuphathiraju Maheswara Varma na kampuni yao Shreeji Enterprises (K) Limited walifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Martha Mutuku.

Katika shtaka la kwanza Bw Soni na kampuni yao wameshtakiwa kwa kudai ushuru wa ziada (VAT) kutoka kwa mamlaka ya KRA ya Sh454,867,754.

Kampuni hiyo pamoja na Bw Soni ambaye ni mkurugenzi  walidaiwa walitekeleza uhalifu huo kati ya Januari 20 na Desemba 20, 2016.

Mahakama ilifahamishwa na kiongozi wa mashtaka kuwa Bw Varma ambaye ni afisa mkuu katika masuala ya fedha ya kampuni hiyo aliisaidia kampuni hiyo kuandaaa vitabu na kudanganya alikuwa ameilipa KRA kodi ya mapato ya Sh980,483,632.

Pia alishtakiwa kudanganya kampuni ya Shreej ilikuwa imelipa ushuru wa VAT Sh454,867,754,

Bw Soni na Shreej walishtakiwa kwa kukataa kulipa ushuru wa VAT Sh261,370,612.

Shtaka lingine dhidi ya Bw Soni na  Shreej ni kuwa alikataa kulipa ushuru wa VAT wa Sh192,997,112.

Kesi itasikizwa Februari 6, 2019.

You can share this post!

Mhadhiri taabani kwa kumtusi Museveni

MUAFAKA: Kamati ya pamoja kuzuru kaunti zote 47 kupata...

adminleo