• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
KCPE: Kakamega yatoa mtahiniwa bora mwaka wa nne mfululizo

KCPE: Kakamega yatoa mtahiniwa bora mwaka wa nne mfululizo

Na PETER MBURU

KAUNTI ya Kakamega, imetoa mtahiniwa bora kote nchini kwa mwaka wa nne mfululizo kulingana na matokeo ya mwaka huu ya mtihani wa darasa la nane (KCPE).

Rawlings Aketch Odhiambo kutoka shule ya msingi ya Hill School Kakamega, aliendeleza rekodi ya kaunti hiyo kutoa mwanafunzi bora kitaifa tangu mwaka wa 2015.

Rawlings, alijizolea alama 453 kati ya 500, alama sawa na za Olive Mwea Wachira kutoka shule ya msingi ya Riara School, Kaunti ya Nairobi ambaye kwa pamoja walichukua nafasi ya kwanza.

Katika mtihani wa mwaka 2017, Goldalyn Kakuya kutoka shule ya msingi ya St Ann Junior School Lubao, katika kaunti hiyo ya Kakamega ndiye aliyeongoza katika mtihani huo kitaifa kwa alama 455.

Mnamo 2016, Oduor Victor Odhiambo kutoka shule ya msingi ya Daisy Special School aling’aa kote nchini kwa kuongoza mtihani wa KCPE alipojizolea alama 437.

Naye Aggrey Akhanyinya kutoka shule ya msingi ya St Joseph Academy iliyoko Kakamega, alikuwa ameibuka mwanafunzi bora kwa alama 449.

You can share this post!

KCPE: Furaha mama wa miaka 68 kuzoa alama 143

KAULI YA WALIBORA: Usiivyoge lugha kimatumizi iwapo...

adminleo