Kimataifa

Wabunge watatu wa upinzani wakamatwa

February 7th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA MASHIRIKA

WABUNGE watatu wa upinzani wamekamatwa nchini Senegal, huku kukiwa na mzozo mkali wa kisiasa.

Mvutano huo ni kufuatia hatua ya Bunge kupiga kura ya kuahirisha uchaguzi wa urais hadi Disemba 15 mwaka huu, hatua iliyotajwa na upinzani kuwa “mapinduzi ya kikatiba”.

Miongoni mwa waliokamatwa ni mbunge Guy Marius Sagna ambaye alijaribu siku ya Jumatatu kuzuia zoezi la kuupigia kura mswada huo.

Msemaji wa chama cha upinzani El Malick Ndiaye alisema ni wazi sasa kwamba Senegal imeingia katika utawala wa kidikteta.

Wakati huo huo, Rais wa zamani wa Chile Sebastián Piñera amekufa jana katika ajali ya helikopta.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Carolina Tohá bila kutoa maelezo zaidi kuhusu chanzo cha ajali iliyotokea katika kusini mwa Lago Ranco.

Piñera, 74 aliiongoza Chile kwa mihula miwili kuanzia 2010 hadi 2014 na 2018 hadi 2022. Viongozi mbalimbali wa Amerika Kusini akiwemo rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wametuma rambirambi wakimtaja kiongozi huyo kama mzalendo aliyekuwa na nia njema kwa taifa lake.