• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 10:55 AM
COFEK yafika mahakamani kupinga sarafu mpya zikiundwa

COFEK yafika mahakamani kupinga sarafu mpya zikiundwa

Na RICHARD MUNGUTI

SHIRIKISHO la Watumizi wa Bidhaa nchini (COFEK) limewasilisha kesi kupinga Benki Kuu ya Kenya (CBK) ikitengeneza sarafu mpya.

Katika kesi iliyowasilishwa katika mahakama kuu Cofek limesema kuwa CBK ilichukua hatua hiyo kabla ya kupata maoni ya umma kuhusu sarafu mpya kwa mujibu wa kifungu nambari 10 cha Katiba.

Kifungu hicho kinasema kabla ya uamuzi wowote kuchukuliwa unaoathiri umma lazima maoni yao yashirikishwe.

Katibu mkuu wa Cofek, Bw Stephen Mutoro amesema katika ushahidi aliowasilisha mahakamani kuwa nembo zinazotumika katika sarafu huwa kielelezo cha cha mshikamano wa kitaifa na lazima maoni ya kila mmoja yashirikishwe.

“Maoni ya wananchi hayakushirikishwa kabla ya nembo mpya kuchapishwa katika sarafu mpya zilizotengenezwa,” amesema Bw Mutoro.

Amesema kuwa CBK haijaruhusiwa kisheria kujitwika jukumu la kuchagua nembo itakayotumika katika sarafu za humu nchini.

“ CBK imewasukumia wananchi nembo hizi pasi kusaka maoni yao kabla ya kupewa fursa ya kueleza hisia zao kabla ya kutengenezwa kwa sarafu hizi,”Bw Mutoro.

Katibu huyo mkuu amesema CBK ilikandamiza haki za kikatiba za wakenya, kutweza uzalendo wao na kuvunja sheria zinazothibiti sarafu za nchi hii.

Akizindua sarafu hizi mpya zitatumika kama ishara kuu kwa turathi za nchi hii na kwamba zitakuwa zakuwaelimisha wananchi na kudumisha utamaduni wa nchi hii na kutumika kutangaza utangamano wa ajabu kwa wakenya.

Alisema CBK itaanza kampeini za kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu sarafu hizi mpya.

Kwa mujibu wa CBK, sarafu hizi mpya zitatumika wakati mmoja na zile za zamani za Marais Jomo Kenyatta, Daniel arap Moi na Mwai Kibaki.

Bw Mutoro amesema Cofek iliandikia CBK mnamo Oktoba 17, akiomba wananchi waulizwe maoni yao lakini benki hii kuu ikakataa.

You can share this post!

Uhuru na Raila washauriana kisiri usiku

Wakazi wamuomba Uhuru avunje Kaunti ya Homa Bay

adminleo