• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 12:46 PM
Wanasiasa Meru wapinga kaunti jirani kupewa Sh1 bilioni za miraa

Wanasiasa Meru wapinga kaunti jirani kupewa Sh1 bilioni za miraa

Na Gitonga Marete

WANASIASA wa Meru wamepinga vikali pendekezo la kutaka kaunti jirani kupewa mgao wa Sh1 bilioni zilizotolewa na serikali kuendeleza kilimo cha miraa.

Viongozi wa kaunti za Embu na Tharaka-Nithi, vilevile, wameshutumu pendekezo hilo kwa kuwatengea kiasi kidogo cha mgao huo.

Kulingana na pendekezo hilo, Kaunti ya Meru inafaa kupewa mgao wa Sh670 milioni, Embu Sh167 milioni na Sh42 milioni kwa wakulima wa Tharaka-Nithi.

Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara wa Miraa wa Nyambene (Nyamita) Kimathi Munjuri aliwataka viongozi wa Meru kukoma kuingiza siasa katika suala la mgao huo wa Sh670 milioni.

Viongozi wa Meru walihoji utaratibu uliotumiwa kugawa fedha hizo kwa kaunti nyingine huku wakisema kuwa hawakushauriwa.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Mpuru Aburi alisema kitita cha Sh1 bilioni kilitolewa na serikali kuu kutokana na shinikizo zilizotolewa na viongozi wa Meru wala si kaunti jirani.

 

You can share this post!

Boinnet achukua hatua kuhusu ulinzi wa mhubiri Owuor

LSK kufika kortini ikitaka DCI akome kukamata washukiwa...

adminleo