Habari za Kitaifa

Pigo lingine kwa Ruto kortini Sheria ya Fedha 2023 ikitajwa kukiuka katiba

Na SAM KIPLAGAT July 31st, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MAHAKAMA ya Rufaa imepiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la Sheria ya Fedha 2023, kwa kukubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu uliotaja sheria hiyo kuwa kinyume na katiba.

Wakikatalia mbali sheria hiyo ambayo ilikuwa na aina mbali mbali za ushuru ikiwemo Ushuru wa Nyumba ambao ulizua vurumai kote nchini, majaji walisema mchakato wa kuunda sheria hiyo ulikuwa na dosari na kwamba ulikiuka Katiba.

“Kwa sababu hiyo, tunatangaza kwamba kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha, 2023 kuwa kulikiuka vifungu 220 (1) (a) na 221 vya Katiba vikisomwa pamoja na Sehemu 37,39A na 40 vya PDMA ambavyo vinaeleza bayana hatua za kutengeneza bajeti, hivyo kufanya Sheria ya Fedha 2023 kuwa kinyume na sheria,”majaji Kathurima M’Inoti, Agnes Murgor na John Mativo wakasema Jumatano, Julai 31.

Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea…