Habari Mseto

Serikali kukopa zaidi mwaka huu

January 10th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Mikopo ya serikali inatarajiwa kuongezeka katika muda wa miezi sita ya mwisho katika mwaka wa kifedha wa 2018/2019.

Hii ni kutokana na kuwa watoaji wa mikopo wanalenga kukopesha serikali zaidi. Huenda ikaathiri ukuaji wa mikopo katika sekta ya kibinafsi kutokana na kuwa huenda benki zisitoe mikopo kwa sekta hiyo.

Hii ni kutokana na kuwa benki huegemea zaidi mashirika yasiyo hatari kwa mikopo. Kutokana na hilo, huenda wamiliki wa biashara ndogo wakaathirika vibaya kwa kukosa mikopo kutoka kwa benki.

Lengo la mikopo ya serikali 2018/2019 ilikuwa ni Sh600 bilioni ila serikali imeshindwa kutimiza lengo la kulipa Sh20 bilioni kati ya Julai na Septemba 2018.

Ripoti iliyotolewa na Cytonn ilionyesha kuwa mikopo iliimarika kwa Sh110 bilioni katika muda huo huku deni la humu nchini likiwa ni Sh60 bilioni ikilinganishwa na deni kutoka nje la Sh50 bilioni.

Lakini serikali ilikuwa imelenga kukopa Sh130.7 bilioni ila ikafeli kutimiza kiwango hicho kwa asilimia 15.