• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Hisia mseto kuhusu pendekezo la kuunganisha kampuni za miwa

Hisia mseto kuhusu pendekezo la kuunganisha kampuni za miwa

Na ELIZABETH OJINA

PENDEKEZO la kuunganisha kampuni tatu za miwa katika eneo la Nyando limepokelewa kwa hisia mseto miongoni mwa wadau katika sekta hiyo.

Kwenye ziara aliyofanya jijini Kisumu mwaka uliopita, Rais Uhuru Kenyatta alipendekeza kuunganishwa kwa kampuni za Chemelil, Muhoroni na Miwani kuwa kiwanda kimoja ili kupata faida.

Chama cha Wakuzaji na Wafanyakazi katika Sekta ya Miwa (KUSPAW) ni miongoni mwa wale wanaounga mkono pendekezo hilo wakisema kwamba litasaidia katika kulainisha baadhi ya changamoto zinazoikumba sekta hiyo.

Mwenyekiti wa chama hicho Francis Wangara alisema kwamba kuunganishwa kwa kampuni hizo kutaziwezesha kuanza kupata faida kubwa.

“Kwa kuwa na viwanda vitatu, kampuni itakayobuniwa itakuwa katika nafasi nzuri kupata faida. Hilo pia linamaanisha kwamba ni sukari ndogo sana ambayo itaingizwa nchini kutoka nchi za nje,” akasema Bw Wangara.

Akaongeza: “Hata hivyo, kubuniwa kwa kampuni kama hiyo si jambo rahisi. Kunahitaji angaa Sh20 bilioni. Ni mpango unaohitaji kuimarishwa kwa viwanda vilivyopo ili kuimarisha utendakazi wao.”

Kulingana na Rais Kenyatta, serikali imetumia hadi Sh30 bilioni kulipa madeni na kufufua viwanda hivyo.

Alisema kwamba hatua hiyo ni mkakati wa kujaribu kupunguza ufujaji wa pesa za umma, hali ambayo imeangusha viwanda vingi.

“Hofu yetu ni kwamba kuunganishwa kwa kampuni hizo tatu kutasababisha baadhi ya wafanyakazi kupoteza ajira zao, kwani si wote watakaopata nafasi kwenye kampuni mpya,” akaeleza.

Baadhi ya wakulima pia wamepinga hatua hiyo. Bw Jerim Odada, ambaye ni mkulima, asema kwamba kampuni hiyo huenda isiwanufaishe wakulima wengi.

You can share this post!

Tiketi za SGR: DPP sasa aitisha faili za Wachina

REKODI YA GUINNESS: Hajanyoa nywele kwa miaka 33 ili apate...

adminleo