• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:10 PM
DUSIT D2: Aliyeponea shambulio la 9/11 Amerika aangamia Riverside

DUSIT D2: Aliyeponea shambulio la 9/11 Amerika aangamia Riverside

Na PETER MBURU

MWANAUME raia wa Marekani ambaye aliponea wakati wa shambulio la bomu nchini Marekani mnamo 2001, almaarufu 9/11, ni mmoja wa watu walioangamia katika vamizi eneo la 14 Riverside Drive, Jijini Nairobi Jumanne.

Jamaa huyo kwa jina Jason Spindler aliuawa Jumanne, baada ya kuponea vamizi la kigaidi miaka 21 iliyopita.

Mamake, Sarah Sandler, alieleza shirika la habari la NBC kuwa mwanaye “alikuwa akijaribu kuleta mabadiliko katika mataifa yanayoendelea, kwenye masoko yanayokua.”

Nduguye Jason, Jonathan naye alidhibitisha kifo cha bwana huyo kupitia mtandao wa Facebook.

“Ndugu yangu Jason Spindler aliaga leo alfajiri wakati wa vamizi la kigaidi Nairobi, Kenya. Jason alinusurika vamizi la 9/11 na ni mpiganaji. Nina hakika kabla ya kufa aliwaonyesha kivumbi,” chapisho la Jonathan likasema.

Serikali ya US ilidhibitisha kuwa raia wao aliuawa katika vamizi hilo.

Spindler aliripotiwa kuwa alikuwa akila chamcha katika hoteli ya Dusit, wakati vamizi hilo lilipotokea.

Alikuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya I-DEV International, ambayo ina makao yake eneo la 14 Riverside, jingo la Belgravia, ghorofa ya sita.

Msimamizi wa kampuni hiyo Afrika Essie Mwikali alidhibitisha kifo cha Spindler, akise wafanyakazi 45 waliokuwa ofisini wakati wa vamizi wote waliponea.

You can share this post!

SHAMBULIO: Wanahabari wa NTV wasimulia hali ilivyokuwa...

UTU: Mwanamke aliyewapa damu watu mahututi mara 61

adminleo