• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 11:14 AM
SHAMBULIO: Polisi wanasa washukiwa 2 wa uvamizi katika hoteli

SHAMBULIO: Polisi wanasa washukiwa 2 wa uvamizi katika hoteli

VALENTINE OBARA Na RICHARD MUNGUTI

POLISI Jumatano waliwakamata washukiwa wawili wa ugaidi wanaoaminika kuhusika katika shambulio la Hoteli ya Dusit D2 jijini Nairobi.

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Bw George Kinoti, alisema wawili hao walikamatwa katika mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi na Ruaka ulio Kiambu.

Hii ilitokea muda mchache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuapa kwamba wote waliosaidia magaidi kufanya mashambulio hayo watakabiliwa vikali.

Wakati huo huo, washukiwa watano wa shambulizi la Chuo Kikuu cha Garissa watajua hatima yao Januari 23, 2019 kwa mauaji ya wanafunzi 144 na maafisa sita wa usalama.

Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani, Bw Francis Andayi alielezwa kuwa washukiwa hao watano walifanya njama za kuwaua wanafunzi hao wakishirikiana na magaidi waliouawa mle ndani na maafisa wa usalama.

Walioshtakiwa ni Mabw Mohammed Ali Abikar, Hassan Edin Hassan, Osman Abdi Dagane na raia wa Tanzania Rashid Charles Mberesero.

Kiongozi wa mashtaka Bi Carol Sigei alimweleza hakimu jinsi kila mmoja wa washukiwa hao aliwasiliana kwa njia ya simu na magaidi waliotekeleza shambulizi hilo.

Lakini wakili Mbugua Mureithi anayewatetea washukiwa hao, aliomba mahakama iwaachilie huru akisema hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya washukiwa.

You can share this post!

SHAMBULIO: Gaidi alikuwa katika WhatsApp ya ‘Nyumba...

SHAMBULIO: Historia ya kikosi cha Recce

adminleo