Dimba

Manchester United sasa waamini Frenkie de Jong ndio atawamalizia shida zao

Na JOHN ASHIHUNDU, MASHIRIKA October 8th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

BARCELONA, Uhispania

MANCHESTER United wanafikiria kufufua mpango wa kumfuatilia Frenkie de Jong, vyombo vya habari za michezo hapa nchini vimeripoti.

United walijaribu kumvutia raia huyo wa Uholanzi mnamo 2022, lakini ikajiondoa katika mpango huo kutokana na bei ghali iliyowekwa mezani.

Lakini sasa Barcelona imetangaza kuwa tayari kumuachilia nyota huyo kwa timu yeyote itakayotoa Sh8.6 Bilioni.

Kiungo huyo ameanza kukatishwa tamaa na maisha ya Barcelona na huenda akanyakuliwa na Chelsea waliotangaza kuwa tayari kumpokea wakati wowote iwapo atakubali kuondoka.

Muda wa Mdachi huyo kuondoka pale Kalalunya umechangiwa na kungangania nafasi katika kikosi cha kwanza ambacho kimejaa viungo wengi wazuri.

Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji wa Barcelona waliosikitishwa na kiwango cha klabuyo hiyo ambayo imepoteza makali kwenye ligi kuu ya LaLiga, Supercopa de Espana na Copa de Rey.

Wakati huo huo, kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, Leroy Sane amesemekana kumaliza utaratibu wote wa kuondoka ili ajiunge na timu nyingine baada ya msimu huu kumalizika.

Mkataba wa staa huyo na klabu ya Bayern Munich utamalizika Juni 30, 2025 na amegoma kuurefusha, huku kukiwa na madai kwamba Arsenal na Newcastle United ni miongoni mwa timu zinazomsaka.

Taarifa zimesema kuwa Newcastle United imekubali kuvenja benki na kuwemamezani kitita kitakachomvutia, huku Arsenal ikiripotiwa kuwa tayari kununua kwa Sh10 bilioni.

Arsenl walikuwa na nia ya kumtwaa mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Ujerumani mnamo 2022, lakini wakajiondoa. Sane amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Munich msimu huu wa 2024/2025.