Habari za Kitaifa

Polisi wa kike kutumwa kwenda kupambana na magenge Haiti kwa mara ya kwanza katika historia

Na NYABOGE KIAGE October 17th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MKUMBO wa kwanza wa polisi wanawake kutoka Kitengo Spesheli cha Silaha na Mbinu (SWAT) kitatumwa Haiti mnamo Novemba.

Huu ndio utakuwa mkumbo wa pili wa zaidi ya polisi 600 ambao watajiunga na wenzao ambao wanadumisha amani nchini Haiti. Polisi 396 ambao wamegawanywa kwenye makundi mawilli tayari wanakabiliana na magenge kule Haiti.

Polisi hao ni sehemu ya kikosi cha kudumisha amani ambacho kinaungwa mkono na Umoja wa Kitaifa (UN).

Hii itakuwa mara ya kwanza ambapo polisi wa kike kutoka Kenya watakuwa wakitumwa kudumisha amani nje ya nchi.

Kwa sasa polisi hao wanaendelea na mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi kwenye bewa la Embakasi A.

Polisi wengine ambao wanatarajiwa kusafiri Haiti ni wale wa GSU, wale wa Kupambana na Wezi wa Mifugo (ASTU) na wale wa kutumwa wakati wa matukio ya dharura (RDU).

Kenya ndiyo inaongoza misheheni hiyo nchini Haiti.