• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
Wazazi wa aliyeaga baada ya kutahiriwa wangali mafichoni

Wazazi wa aliyeaga baada ya kutahiriwa wangali mafichoni

Na David Muchui

MSICHANA aliyefariki kutokana na majeraha ya ukeketaji katika kijiji cha Mwaniki, Igembe ya Kati mwezi moja uliopita bado hajazikwa baada ya wazazi wake kuenda mafichoni.

Msichana huyo alifariki akiuguza majeraha hayo nyumbani kwao mwezi Desemba mwaka jana akiwa pamoja na wenzake waliokwepa mila hiyo.

Naibu Chifu wa Kata ya Kathelwa, Peter Gitonga alieleza TaifaLeo kwamba polisi bado wanawasaka wazazi wa marehemu, Richard Nkonge na Triphosa Kaari waliotoroka baada ya kugundua kwamba walivunja sheria.

Polisi wamekuwa wakikita kambi kijijini humo wakitumai kwamba wawili hao watarejea nyumbani ila hilo halijafanyika.

“Tumesikia kwamba wanajificha mjini Mombasa lakini hawatazuia mkono mrefu wa sheria kuwanasa hata wajifiche wapi,” akasema Bw Gitonga.

Wazazi hao waliwaacha watoto wao wengine chini ya uangalizi wa nyanyao.

You can share this post!

Baba apongeza wanakijiji waliomuua mwanawe mbakaji

KAULI YA WALIBORA: Kanuni ya msingi ya utamkaji izingatiwe...

adminleo