Polo afunguka na kufichulia mke kinachomzuia kuwika kwenye ‘mechi’
MWANADADA wa hapa alimhurumia mumewe jombi huyo alipomwambia kwamba sababu ya kushindwa kwake kutamba chumbani ni kupungukiwa na pesa.
Demu alilazimika kumuuliza mumewe kilichomfanya asiwike tena chumbani tofauti na kawaida yake akishuku alikuwa na mpango wa kando.
Hata hivyo, jamaa alifunguka na kumwambia mkewe kwamba tatizo lake ni mawazo ambayo yanamzonga baada ya mapato yake kupungua.
“Nawaza sana na unajua mapato yamepungua. Hali hii imeniathiri pakubwa na itabidi unielewe. Sijawahi kufikiria kuwa na mpango wa kando katika maisha yangu,” jamaa alisema na mkewe akamhurumia na kumwambia asijiumize sana kimawazo.