Mke azaba mumewe kofi kali kwa kupiga gumzo la mhudumu wa duka
KIZAAZAA kilizuka katika supermarket moja mtaani hapa Makongeni, Thika, jamaa alipozabwa kofi na mkewe kwa kumezea mate kidosho aliyehudumu katika duka hilo.
Duru zinasema kuwa, wawili hao walifika katika duka hilo kununua bidhaa jamaa alipojitenga na mkewe.
Katika pilkapilka za kumsaka, demu alimfumania jamaa akipiga gumzo na kipusa mmoja pembeni. Alipowaona alienda kumfokea jamaa mbele ya wateja wengine na kumzaba kofi.
“Ulikuja kutongoza wanawake hapa ama kununua bidhaa? Na wewe msichana, unaongea na mume wangu kama nani. Unanijua? Ninaweza kukuharibu hiyo sura yako sasa hivi,” mke wa jamaa alisema.
Hata hivyo, jamaa alikanusha madai ya mkewe na kumlaumu kwa kuzua sarakasi.