• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:21 PM
Polisi wanasa watu 6 wanaoshukiwa kufadhili magaidi

Polisi wanasa watu 6 wanaoshukiwa kufadhili magaidi

NA MAUREEN KAKAH

MAHAKAMA itaaamua iwapo itawaachilia kwa dhamana washukiwa wengine saba wa ugaidi wanaohusishwa na shambulizi la kigaidi la hoteli ya DustinD2 lililosababisha vifo vya watu.

Washukiwa hao Hassan Abdi Nur, Ismael Sadiq Abitham, Ali Khamisi Ali, Abdinoor Maalima Osmail, Abdullahi Muhumed Hassan na Sophia Njoki Mbogo Jumatano walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya Milimani, Martha Mutuku.

Kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi (ATPU) kilifahamisha mahakama kwamba,, washukiwa hao walikamatwa Jumanne katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi. Sita hao wanashukiwa kwamba walifadhili shambulizi hilo la DustiD2 kati ya Januari 15 na Janauari 16.

“Imetimu saa kumi na moja jioni na mawakili sasa watawasilisha maombi yao mahakamani kabla ya saa sita kesho kwa sababu kuna mwelekeo kwamba hatuwezi kuendelea baada ya saa kumi na moja jioni. Naamrisha washukiwa wazuiliwe katika makao makuu ya ATPU,” akasema Bi Mutuku.

Mahakama ilielezwa kwamba, mshukiwa Bw Nur anaendesha biashara ya M-Pesa kupitia kampuni ambayo jina lake lilibanwa ili kuzuia kuvurugwa kwa uchunguzi.

Bw Nur alisajili akaunti 47 za M-Pesa mnamo Oktoba 2018 kati ya akaunti zote 52 alizozisajili mwaka huo. Cha kushangaza ni kwamba, simu mbili pekee zilitumika kusajili akaunti hizo japo vitambulisho tofauti vilitumika.

Bw Nur pia alipokea fedha nyingi kutoka Afrika Kusini na pesa hizo zilitolewa kupitia nambari maalumu ya kutoa pesa katika benki ya Diamond Trust kisha kutumwa kwa watu fulani nchini Somalia baada ya mawasiliano mara kadhaa ya simu.

Mshukiwa wa pili, Bw Abitham naye alikuwa akizungumza na mshukiwa mkuu aliyeuawa Ali Salim Gichunge na mkewe anayeandamwa na polisi Violet Omwoyo Kemunto.

Bw Ali, ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika runinga ya Horizon naye anadaiwa kuwasiliana na watu kutoka Somalia wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Alshabaab.

Washukiwa wengine Mabw Osmail, Hassan na Mbogo nao walipokea Sh100 milioni, kuwapa vidokezo na kuhakisha fedha zilizotumwa zinawafikia magaidi.

You can share this post!

Uteuzi wa Matiang’i tumbojoto kwa wandani wa Ruto

TAHARIRI: Maafisa waimarishe doria katika mipaka

adminleo