Polo asutwa kwa kukejeli demu mnene aliyejaza pikipiki nzima!
LULUNG’A, NAROK
POLO wa hapa alisutwa vikali na kipusa mmoja kwa kudinda kupanda pikipiki wabebwe pamoja kwa madai kuwa kipusa huyo alichukua nafasi yote.
Duru zinaarifu polo alikuwa akitembea barabarani mwanabodaboda aliposimamisha pikipiki na kumwomba awe mteja wake.
“Ni kweli ninataka kupanda pikipiki lakini huoni huyu mrembo hajaacha nafasi? Acha kipusa ajikweze kwa raha zake kwani mwili wake hutaka nafasi kubwa,” jombi akasema.
Mrembo aliudhika na akamzomea polo vikali.
“Una haja gani na mwili wangu? Unikome kabisa. Hata unaweza kununua pikipiki yako!” kipusa alimchemkia jamaa kwa hamaki.