• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 1:14 PM
Murathe ashauri Kalonzo apuuze ‘kelele’ za waasi katika Wiper

Murathe ashauri Kalonzo apuuze ‘kelele’ za waasi katika Wiper

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Naibu Mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe amemshauri kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kupuuza ‘kelele’ za waasi katika chama chake na kulenga umoja wa eneo la Ukambani.

Akiongea eneo la Yatta, Kaunti ya Machakos nyumbani kwa Bw Musyoka, Bw Murathe alidai waasi wa Wiper wanaeneza uvumi kuwa makamu huyo wa zamani wa Rais ameshindwa kuongoza jamii yake, ili inufaike na mgawanyiko katika Wiper.

“Nimesikia maneno huko nje watu fulani wakisambaza propaganda kuwa Kalonzo hatoshi na sisi tunamtambua kama kiongozi anayesaidia Rais Uhuru Kenyatta kupigana na ufisadi na kuleta umoja nchini,” alisema Bw Murathe.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na kiongozi wa chama cha New Democrats Party Lloyd Masika, wabunge Nimrod Mbai (Kitui Mashariki), Boni Mwalika (Kitui Mashambani), na Erastus Kivasu (Mbooni).

Bw Musyoka alisisitiza umuhimu wa umoja wa Ukambani na kuonya kunyima jamii nafasi ya kupata urais iwapo mgawanyiko utaendelea.

 

You can share this post!

Gari la mwanamke aliyeuawa kinyama lapatikana

Wabunge waitaka NCPB iwaondolee wakulima masharti

adminleo