Shangazi Akujibu

Mke wangu alifariki, je ni sawa nikioa dada yake?

Na PAULINE ONGAJI January 23rd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

Shikamoo shangazi? Mke wangu alifariki miaka miwili iliyopita na kuniachia watoto watatu. Sasa dada ya mke wangu ambaye ni shemeji yangu, anataka nimuoe. Inakubalika?

Marahaba!

Kuna jamii ambazo huruhusu hili kama njia ya kuhakikisha kwamba watoto wa marehemu wanalelewa na jamaa wa karibu. Lakini sidhani huu ni uamuzi wa busara. Kumbuka hisia za mapenzi kwake si sawa na ulizokuwa nazo kwa mkeo. Tulia uwalee wanao kwa sasa na wakati ufaao ukifika utakutana na yule mnayependana naye.