• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
KANU yasifu agizo la Rais kukomesha siasa za 2022

KANU yasifu agizo la Rais kukomesha siasa za 2022

Na Stephen Munyiri

CHAMA cha KANU, tawi la Kaunti ya Nyeri kimemsifu Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwasuta viongozi wanaoendeleza kampeni za mapema badala ya kufanya maendeleo.

Kwenye taarifa iliyotolewa na katibu wa chama katika tawi hilo, Bw Michael Kiruki Karonji baada ya mkutano wao Jumamosi, chama hicho kilisema kitengo kilichopata umaarufu wa ‘Tangatanga’ katika Chama cha Jubilee kilihatarisha sifa ya Rais Kenyatta kama hakingezuiliwa.

“Wameanzisha kampeni za mapema za urais na kupuuza wito wa mara kwa mara wa rais kwamba siasa zikomeshwe. Rais asiruhusu chochote kuzuia ajenda yake,” akasema Bw karonji.

Katika siku za hivi majuzi, Rais Kenyatta amezidi kuonya wanaofanya siasa za 2022 akisema walio serikalini na hawataki kufuata agizo hilo wajiuzulu.

Hii ni kutokana na kuwa rais anatazamia kutekeleza ajenda zake za maendeleo kabla akamilishe uongozi wake wa awamu ya pili iliyo ya mwisho 2022.

 

You can share this post!

SENSA: Jamii za kuhamahama zaombwa kujitokeza kuhesabiwa

Magavana 40 waliajiri mawaziri bila kuzingatia sheria...

adminleo