
Wanandoa wanaoonekana kukosana. PICHA|HISANI
SWALI: Hujambo shangazi? Nina mke na watoto watatu. Kuna tatizo limetokea katika ndoa yangu.
Siku za hivi majuzi mke wangu huwa hanitaki chumbani na ninalazimika kulala chumba kingine. Nifanye nini?
JAWABU: Hatua ya mke wako ya kukufukuza katika chumba chenu inakiuka mipaka na inakupa sababu nzuri ya kuvunja ndoa hiyo.
Keti naye chini akwambie sababu. Kama amechoka na ndoa, ni vyema ujue hivyo ili muachane.