• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
HELLEN NUNGARI: Mwigizaji wa lugha ya Gikuyu anayelenga makuu

HELLEN NUNGARI: Mwigizaji wa lugha ya Gikuyu anayelenga makuu

Na JOHN KIMWERE

ISINGEKUWA ni majaliwa ya Maulana, Hellen Nungari Mwaura hangetokea kuwa nyota katika tasnia ya filamu na muvi ambazo hupeperushwa kwa lugha ya Gikuyu maana tangu utotoni mwake alipania kuwa mhasibu.

Je, alijipataje hapa? Mwanzoni, binti huyu hakuwa na hata chembe za talanta hiyo, lakini nyota yake ilimwangazia alipoandamana na kakake, Simon Mwaura kuhudhuria majaribio ya uigizaji mjini Gatanga, Kaunti ya Murang’a.

”Mwaka 200 nilisindikisha kakangu kuhudhuria majaribio yaliyoandaliwa na kundi lililoitwa Ventures Arts, lakini ilitokea kama muujiza badala yake nilichukuliwa mimi,” alisema na kuongeza alishauriwa ndiye alionyesha vigezo vya uigizaji.

Anadai ingawa hadi sasa huona soni kuzungumza mbele ya watu aliibuka kati ya wateule bora baada ya kuonyesha angefana katika tasnia ya filamu.

”Ingawa Ventures Arts haikudumu, kipindi hicho nilianza uigizaji na kundi la UJ15,” alisema. Kipusa huyu ambaye katika sanaa anafahamika kwa majina tofauti kama ‘Wagachara,’ ‘Muthoni,’ ‘Wagithomo,’ ‘Gathoni’ na ‘Njambi’ amepiga hatua kubwa katika sekta hiyo ingawa anadai ana malengo pia safari bado ndefu kufika anapotaka.

Alibahatika kunoa kipaji chake kutokana na vitabu vinayotahiniwa katika elimu ya sekondari almaarufu ‘setbooks’ kuandaa shoo za uigizaji kupitia makundi mbalimbali na kufika alipo. Hayo tisa. Kumi dada huyu ameshiriki kazi chungu zima za uigizaji na kurushwa kupitia vituo tofauti ikiwamo ‘Nyumba ya Mumbi TV,’ ‘Njata TV,’ ‘Kameme TV,’ na ‘Inooro TV.’

”Nimepiga shughuli za uigizaji na makundi mengi ndani ya miaka kumi iliyopita na kujizoela umaarufu mkubwa hali ambayo hunipa ajira zaidi,” akasema.

Mrembo huyu hushiriki filamu moja series na muvi mbili ambazo

hurushwa kupitia Inooro TV. Chini ya produsa John Marete, hushiriki filamu inayoitwa ‘Micii ni Ndogo series (familia ni ndogo) ambapo ndiye Njambi.

Pia uigiza muvi mbili tofauti (Central Cinema) chini ya Advanced Pictures na Israel Production anakojulikana kama Gathoni na Muthoni mtawalia.

Kati ya mwaka 2015 na 2016 alifanikiwa kushiriki filamu ya Ploti series iliyopeperushwa kupitia Jata TV akijulikana kama Wagithomo.

Aidha ameshiriki muvi zinginezo nyingi ikiwamo ‘Hinya wa Mahoya,’ chini ya kundi la Rupian Production pia ‘Magerio’ iliyotengenzwa na Furet Films na kurushwa na Kameme TV. Anasistiza kwamba ameshiriki filamu nyingi tu ambazo zimeshamtoka akilini.

Dah! Usikonde. Nungari (30) anafunguka kwamba anapania kuanzisha familia hivi karibuni na Mungu ambapo atahitaji amjalie watoto watatu.

Mwigizaji huyu mmiliki wa kampuni ya Hellen Hikes Adventures anasema licha ya kwamba katika ni mitego mitupu anapania kufikia mafanikio ya juu. Anataka kuibuka kati ya watengenezaji muvi sifika nchini hasa kufikia kiwango cha veterani Betty Kathungu Furet.

Dada huyu ameamua kujikaza kisabuni kufuata njia za veretani na staa wa Nollywood, Mercy Johnson. Msanii huyo wa filamu za Kinigeria amefaulu kunasa tuzo tele kuhusiana na fani hiyo.

Anasema kuwa staa wengi hudhania tayari amefika kiwango cha kusaidia wasanii wanaokuja hasa kuwapa ajira. Anaamini atafunguliwa milango zaidi kuendeleza talanta katika fani hiyo. Hata hivyo mwana dada huyu siyo mchoyo. Anashauri waigizaji chipukizi waache pupa bali wawe wakuvumilia na kumtumaini Mungu kuwapigania nyakati zote.

You can share this post!

FILAMU: Spellancer Nancy wa Inspekta Mwala alenga kuanzisha...

IRENE KIENDI: Mwigizaji wa Viusasa nguli wa filamu za...

adminleo