Habari

Watu kuutazama mwili wa Baba Kasarani

Na WINNIE ONYANDO October 16th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

ENEO la kutazama mwili wa Kiongozi wa Chama cha ODM, Raila Odinga limegeuzwa kutoka Bunge la Kitaifa hadi Kasarani.

Hii ni baada ya wafuasi au waombolezaji kujaza bungeni wakisubiri kutazama mwili wa kiongozi huyo mashuhuri.

Umati mkubwa pia ulishuhudiwa katika uwanja wa ndege wa JKAI huku kila mmoja akitoa heshima zake za mwisho kwa Baba.

Hii ilifanya pia serikali kuhairisha mango wa kuusafirisha mwili wake hadi katika makafani ya Lee Funeral Home.

Maamuzi hayo yanajiri baada ya umati mkubwa kujitokeza kuusindikiza mwili wa Raila kutoka JKIA, huku kundi jingine likielekea Bungeni.

Wale ambao tayari walikuwa wameanza kupanga foleni Bungeni wameshauriwa kuelekea kwenye Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Kasarani.

Tayari barabara ya Thika Road imefurika umati na magari watu wakielekea Kasarani.