Man United yauma nje tena kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ya kocha Thomas Tuchel
MASHABIKI wa United wanalia hakuna tena mchezaji hata mmoja kwenye timu ya taifa ya Uingereza baada ya kocha Thomas Tuchel kutangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa michuano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Serbia na Albania.
Kukosekana kwa mchezaji wa United kumezua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki na wachanganuzi, baada ya Mjerumani huyo kutangaza wachezaji wake wapya kuelekea raundi ya mwisho ya mechi.
Jude Bellingham, Phil Foden, Adam Wharton na Nick Pope wote wamerejea kikosini, huku kiungo chipukizi wa Bournemouth, Alex Scott, akiitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya watu wazima baada ya kuonyesha ustadi katika Ligi Kuu.
Hata hivyo, kutojumuishwa kwa Jack Grealish (Everton) na Trent Alexander-Arnold (Real Madrid) kumezua maswali zaidi, huku chipukizi wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly, pia akikosa nafasi.
La kushangaza ni kwamba Tuchel ameamua kutojumuisha mchezaji hata mmoja wa Manchester United, akitaja sababu za kiwango na uwiano wa kimbinu kama msingi wa maamuzi yake.
Wakati huohuo, Bellingham kutoka Real Madrid amerejea kikosini baada ya kupona majeraha, na Foden wa Manchester City anatarajiwa kuwa mchezaji muhimu katika mipango ya Tuchel.
Uingereza tayari wamejihakikishia tiketi ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kutawala mechi zote sita za kwanza za kufuzu, na sasa watamenyana na Serbia katika uwanja wa Wembley mnamo Novemba 13 kabla ya kusafiri jijini Tirana hapo Novemba 16 kupepetana na Albania, huku Tuchel akilenga kudumisha kasi na kuimarisha kikosi chake kuelekea Kombe la Dunia 2026 nchini Amerika, Canada na Mexico.
Kikosi cha Uingereza:
Makipa – Dean Henderson (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton), Nick Pope (Newcastle United);
Madifenda – Dan Burn (Newcastle United), Marc Guehi (Crystal Palace), Reece James (Chelsea), Ezri Konsa (Aston Villa), Nico O’Reilly (Manchester City), Jarell Quansah (Bayer Leverkusen), Djed Spence (Tottenham Hotspur), John Stones (Manchester City);
Viungo – Elliot Anderson (Nottingham Forest), Jude Bellingham (Real Madrid), Jordan Henderson (Brentford), Declan Rice (Arsenal), Morgan Rogers (Aston Villa), Alex Scott (Bournemouth), Adam Wharton (Crystal Palace);
Washambulizi – Jarrod Bowen (West Ham), Eberechi Eze (Arsenal), Phil Foden (Manchester City), Anthony Gordon (Newcastle United), Harry Kane (Bayern Munich), Marcus Rashford (Barcelona, loan from Manchester United), Bukayo Saka (Arsenal).