Mchujo wa kufa kupona kati ya timu ya Nigeria, Gabon na Cameroon, DR Congo
TAYARI timu tisa za Kanda ya Afrika zimefuzu moja kwa moja kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026.
Hata hivyo, timu nne- Nigeria, Gabon, Cameroon na DR Congo zinarejea uwanjani Novemba 13, 2023 nchini hapa kuendelea na mchujo wa kufuzu fainali hizo zitakazofanyika nchin Amerika, Canada na Mexico.
Katika mechi hizo, Nigeria imepangiwa kukutana na Gabon kuanzia saa mojajioni, wakati Cameroon ikipambana na DR Congo kuanzia saa nne usiku.
Washindi watakutana kwenye fainali hapo Jumapili (Novemba 16) kutafuta nafasi ya kushiriki mchujo mwisho dhidi ya timu kutoka mabara mengine kuwania tiketi ya mwisho ya kufuzu kwa Kombe hilo Dunia.
Timu hizo zilifuzu kwa mchujo wa Kanda Afrika baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi ya kuwania kufuzu kwa Kombe hilo la Dunia.
DRC Congo ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B, wakati Cameroon ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D.
Nigeria ilishika nafasi ya pili nyuma ya Afrika Kusini katika Kundi C wakati Gabon ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi E.
Katika mechi ya leo (Novemba 13, 2025), Pierre-Emerick Aubameyang anayechezea klabu ya Marseille atarejea katika kikosi cha Gabon baada ya kumaliza adhabu ya kulishwa kadi nykundu iliyomfanya akose mechi ya Kundi dhidi ya Burundi.
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal alifunga mabao yote manne katika ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Gambia jijini Nairobi mnamo Oktoba 10, ushindi ulioiwezesha Gabon kumaliza miongoni mwa timu nne bora kwenye makundi tisa ya kufuzu.
Katika viwango vya kimataifa vya FIFA, Nigeria wanashikilia nafasi ya 41, wakati Gabon chini ya kocha Thierry Mouyouma wakikamata nafasi ya 77.
Cameroon wanaonolewa na Marc Brys wanashikilia nafasi ya 54 kwenye msimamo huo, wakati DR Congo chini ya Sebastien Desabre wakikamata nafasi ya 60
Kocha Eric Chelle wa Nigeria amethibitisha kwamba kikosi chake kimejiandaa vyema kwa mchujo huu, licha ya uvumi unaoenea kwamba wamezuzia mazoezi tangu waingie kambini nchini Morocco mapema wiki hii.