Eze aiadhibu Spurs baada ya kugoma kujiunga nao Agosti
KIUNGO mshambuliaji Eberechi Eze aliwaadhibu Tottenham Hotspur katika debi ya London Kaskazini Novemba 23, 2025 jioni, na kuisaidia Arsenal kufungua mwanya wa alama sita kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).
Arsenal iliinyorosha Spurs 4-1 ugani Emirates ambapo, Eze alifunga mabao matatu “hat-trick” dakika ya 41, 46 na 76 nae Leandro Trossard akacheka na wavu dakika ya 36. Bao la kufutia machozi la wenyeji lilitiwa kimiani na Andre Richarlison dakika ya 55.
Eze 28, raia wa Uingereza tangia utotoni amekuwa shabiki hakiki wa Arsenal na alijua siku moja ataisakatia klabu hiyo. Lakini mapema msimu huu, alihusishwa na uhamisho wa kujikunga na Spurs lakini dili hiyo iligonga mwamba baada ya Spurs kushindwa kufika bei.
Mnamo Agosti 20, siku mbili kabla ya uhamisho wa Eze kwenda Arsenal kuthibitishwa, mchezaji huyo alionekana kuwa na uhakika wa kujiunga na Tottenham.
Maji yalizidi unga na alichagua Emirates kwa uhamisho wa Sh 7.7 billioni (£60 milioni) kwenda Emirates kutoka Crystal Palace.
Kabla ya kichapo hicho, kocha wa Spurs Thomas Frank aliulizwa kuzungumzia kuhusu kukosa kumsajili Eze, kocha huyo aliwajibu wanahabari kwa kuuliza “Eze ni nani?”. Aliendelea akisema, “Eze ni mchezaji mzuri wa Arsenal amabo tunatakaa kuwakaanga Jumapili.”
Mnamo Agosti akimpiga kijembe Eze baada ya pia kumkosa Morgan Gibbs-White kutoka Nottigham Forest, Frank aliendelea: “Na ili kuweka wazi kabisa, sitaki wachezaji wowote ambao hawataki kuja kwenye klabu, hatuwataki hapa.”
Matamshi yake sasa yalimrudia. Haikuwa mara ya kwanza kwa Mdenmark huyo kumzungumzia Mwingereza huyo tangu dirisha la uhamisho lifungwe.
Matokeo hayo yanaacha Arsenal ikiwa pointi sita mbele ya Chelsea na saba mbele ya Manchester City, huku Spurs ikiwa nafasi ya tisa, pointi 11 nyuma ya Gunners.
Katika mechi nyingine, Mabao mawili ya Morgan Rogers katika kipindi cha pili, yaliisaidia Aston Villa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Leeds United uwanjani Elland Road.
Rogers alikuwa amefunga bao moja tu EPL msimu huu kabla ya mechi ya Jumapili, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alirejesha kiwango chake bora kutoka 2024/25 na kuongoza timu ya Unai Emery kupata ushindi.
Leeds walikuwa wameongoza mapema wakati bao la Lukas Nmecha lilinusurika ukaguzi wa VAR, ingawa Rogers alirejesha bao dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Wanapanda hadi nafasi ya nne kwenye jedwali na alama 21, pointi nane nyuma ya Arsenal. Wakati huo huo, Leeds walishuka hadi nafasi ya 18 na alama 11.
Matokeo ya jana
Leeds 1-2 Aston Villa
Arsenal 4-1 Spurs