Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Majukumu yanilemea
Mwanaume anayekabiliwa na msongo wa mawazo. Picha|Maktaba
SWALI: Hujambo shangazi. Nilianza kazi miezi michache iliyopita. Nilipolipwa mshahara wa kwanza, bili za nyumba zilimeza pesa zote. Naona heri niache kazi nirudi niishi na wazazi. Nipe ushauri.
Jibu: Sioni kama hatua hiyo itakusaidia. Usirudi kuishi na wazazi. Endelea na kazi ili ujifunze kujitegemea. Baada ya muda mambo yataanza kunyooka.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO